Kabla ya mchezo wa robo fainali kombe la FA dhidi ya Mwadui Fc, ilitolewa taarifa ya kukosekana kwa baadhi ya wachezaji kutokana na sababu mbalimbali
Miongoni mwa wachezaji hao, Michael Sarpong, Lamine Moro na Metacha Mnata walikosekana kutokana na makosa ya utovu wa nidhamu
Sarpong nae ni mtovu wa nidhamu! huyu nafasi yake si apewe Kaseke tu
Yaani kocha Nasreddine Nabi anaweza kumuanzisha Deus Kaseke kama mshambuliaji wa kati akawa na madhara kuliko Sarpong!
Ndio! Kaseke amefunga jumla ya mabao nane (Ligi na FA) msimu huu pamoja na kutoa pasi za mabao matano kwenye ligi
Idadi hiyo ni mara mbili ya mabao yaliyofungwa na Sarpong ambaye eti ni mtovu wa nidhamu!
Kaseke ana sifa zote za mshambuliaji, angalia bao la pili alilofunga dhidi ya Mwadui Fc leo!