Mabao mawili yaliyofungwa na Deus Kaseke, yameipeleka Yanga nusu fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) baada ya kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Mwadui Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga
Kikosi cha Yanga chini ya kocha Nasreddine Nabi kimeendelea kuimarika zaidi leo wakicheza kandanda safi huku wakitengeneza nafasi nyingi
Kukosekana kwa umakini, kumeinyima Yanga ushindi mnono zaidi
Kaseke alifunga bao la kwanza kwenye dakika ya 25 akitumia makosa ya mlinda lango wa Mwadui Fc

Katika dakika ya 57, 'Mwaisa mtu mbad' akaweka kambani bao la pili baada ya kutengewa pasi ya kichwa na pacha wake Yacouba Songne
Songne aliifungia Yanga bao dakika chache baadae akimalizia krosi ya Kaseke lakini mwamuzi msaidizi akafanya yake licha ya kuwa hakukuwa na offside yoyote
Ni ushindi ulioipeleka Yanga nusu fainali sasa wakitarajiwa kuwakabili Biashara United katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mkoano Tabora
Yanga na Nabi inaupigwa 'mwingi', timu inatengeneza nafasi kwa wingi, changamoto iko kwenye matumizi ya nafasi hizo