Beki kisiki Vicent Bossue aliipa Yanga masharti ambayo uongozi uliona hayatekelezeki hivyo kumruhusu akatafute mahali pengine kama ilivyokuwa kwa Niyonzima.
Mchezaji huyo alitegemea kama mambo yatashindikana Yanga basi angetua Singida United iliyokuwa imemuahidi kumpa mkataba mnono.
Kocha wa Singida United Hans van Pluijm ndiye aliyekuwa ameagiza mchezaji huyo asajiliwe.
Sasa Singida United imeachana na mpango wa kumsajili beki huyo raia wa Togo vyanzo vyetu vikieleza sababu ni mahitaji yake kuwa juu.
Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga amekiri kuwa mwanzoni walikuwa na mipango na mchezaji huyo, lakini wameamua kuachana nae huku akidai wamemaliza usajili wa wachezaji wa kigeni.
"Tushakamilisha jumla ya wachezaji saba wa kigeni katika kikosi chetu, kwahiyo hatutakuwa tena na mahitaji na Bossou ingawa alikuwa yupo katika mipango yetu," alisema Sanga.
Beki huyo alitaka Yanga impe dau la usajili la dola 42,000(Mil 92), mshahara wa dola 4,200 (Sh milioni 9.2), tiketi mbili za ndege kila mwaka kwa ajili ya yeye na mkewe wakati wa mapumziko pamoja na bonasi ya dola 5,000 (Sh milioni 11) timu ikitwaa ubingwa.
Kuna taarifa Bossou yuko nchini Afrika Kusini kufanya majaribio klabu ya Bidvest Wits.

ADVERTISE HERE