Job amejibu maswali ya wengi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
23 May 2021
Job amejibu maswali ya wengi

Usitishwe na umbile lake, mlinzi Dickson Job ni moja ya usajili makini ambao Wanayanga wanaweza kujivunia

Alikuwa Cedric Kaze, mkufunzi wa zamani wa Yanga aliyependekeza mlinzi huyu mwenye umri wa miaka 20 tu asajiliwe kutoka klabu ya Mtibwa Sugar

Kaze alimsajili Job huku akiwa na safu ya ulinzi imara eneo la kati iliyowajumuisha manahodha Lamine Moro na Bakari Nondo Mwamnyeto pamoja na Abdallah Shaibu 'Ninja' na Said Juma Makapu

Wapo waliohoji kwa ukuta huu Job amesajiliwa wa nini Yanga?

Lakini baada ya kucheza takribani mechi tano, Job amejibu maswali ya wengi

Hakuwa na mwanzo mzuri kwani alilazimika kusubiri takribani miezi mitatu kucheza mechi yake ya kwanza kutokana na majeraha

Job ni mlinzi anayetumia akili zaidi kuliko nguvu. Yuko vizuri mguuni, pasi makini na hodari wa kusoma mchezo

Utashangazwa na uwezo wake wa kucheza mipira ya juu. Katika mchezo wa ligi kuu uliopita dhidi ya JKT Tanzania ambao Yanga walishinda kwa mabao 2-0, Job ndiye alicheza mipira mingi ya kichwa mbele ya washambuliaji warefu wa JKT Tanzania wakiongozwa na Dani Lyanga

Job ni mchezaji kiraka, kwani pamoja na kumudu vyema safu ya ulinzi wa kati, Job anaweza kucheza kama mlinzi wa pembeni au kiungo mkabaji

Yanga wanamkosa nahodha Lamine Moro ambaye bado anasubiri ufumbuzi wa suala lake na benchi la ufundi, lakini hakuna hofu katika safu ya ulinzi

Wananchi wanafahamu wana Job, Nondo na Makapu na wakati huo wakisubiri Ninja apone majeraha ambayo yamemuweka nje kwa wiki mbili sasa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
4h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
17h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
22h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’