Pamoja na Simba kutolewa robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa kwa kufungwa mabao 4-3 lipo jambo ambalo wamelifanya katika michuano hiyo ambalo bila shaka ni mithani kwa viongozi wa Yanga
Msimu ujao Yanga itashiriki michuano ya CAF, kama watakuwa mabingwa au kumaliza nafasi ya pili watacheza ligi ya mabingwa lakini pia kama watamaliza nafasi ya tatu au kutwaa ubingwa wa kombe la FA watashiriki kombe la Shirikisho
Mechi za awali zinatarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi August hivyo ni wazi Wananchi wanapaswa kuanza maandalizi yao mapema baada ya ligi kumalizika
Aidha Yanga inahitaji kuboresha kikosi chake ili kuwa na ushindani wa kweli katika michuano hiyo kama walivyofanya watani zao msimu huu
Miaka ya karibuni Yanga imecheza mara kadhaa hatua ya makundi ya michuano ya kombe la Shirikisho lakini hawakuwahi kuvuka hatua hiyo
Mara ya mwisho Yanga kutamba ilikuwa mwaka 1998 ambapo walitinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa wakati huo hatua ya makundi ikishirikisha timu nane
Kwa uwekezaji ambao unaendelea kufanyika, umefika wakati Yanga kama walivyo watani zao kuanza kutikisa soka la Afrika
Uzuri tayari wanaye kocha Nasreddine Nabi ambaye amewahi kushinda ubingwa wa kombe la Shirikisho barani Afrika, huyu anafahamu aina gani ya wachezaji anawahitaji na maandalizi ili kuweza kufanya vizuri kwenye michuano hiyo