Jumanne ya wiki ijayo, May 25 Yanga watakuwa Shinyanga kumenyana na Mwadui Fc ukiwa ni mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC)
Wananchi wameweka kambi Singida kujiandaa na mchezo huo ambao matokeo ya ushindi yatawapeleka nusu fainali kwa msimu wa pili mfululizo
Msimu uliopita Yanga iliishia hatua ya nusu fainali wakifungwa na watani zao Simba mabao 4-1
Msimu huu Yanga imepania kuvuka hatua hiyo na lengo mama likiwa kutwaa ubingwa ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki michuano ya CAF msimu ujao
Pamoja na kuwa kimahesabu, mpaka sasa Yanga inaweza kushiriki michuano ya CAF msimu ujao kama Tanzania itapewa nafasi nne kulingana na msimamo wa ligi
Simba, Yanga na Azam Fc tayari zimejihakikishia nafasi tatu za juu ambazo zitatumika kutoa timu tatu kati ya nne ambazo zitashiriki michuano ya CAF
Timu ya nne ikiwa bingwa wa kombe la Shirikisho au timu itakayoshika nafasi ya nne kama bingwa wa Shirikisho atakuwa moja kati ya timu hizo zilizo juu ya msimamo
Pamoja na kuwa Wananchi bado hawajakata tamaa na mbio za ubingwa wa ligi kuu, lakini huku kwenye Shirikisho wana nafasi kubwa zaidi ya kutinga fainali na pengine kuwa mabingwa
Kama Yanga itashinda dhidi ya Mwadui Fc, mchezo wa nusu fainali itacheza na mshindi wa mchezo kati ya Biashara United dhidi ya Namungo Fc
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Ali Hassan Mwinyi, Tabora