Tuisila Kisinda 'TK Master' ni winga anayewakumbusha wananchi enzi za kila Said Maulid 'SMG', Edibily Lunyamila, Simon Msuva na wengineo waliopita Yanga na kupata mafanikio wakiwa washambuliaji wanaotokea pembeni
Silaha kubwa ya Kisinda ni kasi, hakuna shaka kwenye ligi, yeye ndiye mchezaji mwenye kasi zaidi
Akiwa katika maeneo yake sio kazi rahisi kupimana nae ubavu kwenye mbio
Jana alifunga bao lake la tano msimu huu ambao pia ametoa pasi tano za mabao
Huyu mwamba akifungua turbo ni mateso kwa walinzi wa timu pinzani!
ADVERTISE HERE