Mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) dhidi ya Mwadui Fc utapigwa Jumanne ijayo, May 25 katika uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga
Ratiba iliyotolewa na TFF mapema leo, imebainisha kuwa mechi zote za robo fainali zitapigwa May 25/26 2021
Aidha michezo ya nusu fainali itapigwa mikoa ya Ruvuma na Tabora
Nusu fainali ya kwanza itahusisha mshindi wa mchezo kati ya Simba vs Dodoma Jiji dhidi ya Rhino Rangers vs Azam Fc. Mchezo huu utapigwa Songea
Nusu fainali ya pili itahusisha mshindi wa mchezo kati ya Biashara United vs Namungo Fc dhidi ya Mwadui Fc vs Yanga
ADVERTISE HERE