May 08 Yanga ilichukua uamuzi mgumu wa kususia mchezo dhidi ya Simba uliopaswa kupigwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Ulikuwa uamuzi sahihi kuchukuliwa kwani mpira wa miguu lazima uendeshwe kwa kanuni na taratibu zake
Haiwezekani siku ya mchezo saa mbili kabla muda unabadilishwa pasipo kuheshimu kanuni hizo
Bodi ya ligi imetangaza tarehe nyingine ya mchezo huo kupigwa (Julai 03)
Bado Wanayanga wengi wao hawaoni sababu ya viongozi wao kupeleka timu uwanjani kwani tayari walishafanya hivyo kwa mujibu wa kanuni
Aidha, waliosababisha kadhia ile wanapaswa kuwajibika ili siku nyingine waheshimu kanuni na taratibu zilizowekwa
Tukio la May 08 ni kama limemalizwa kisiasa tu baada ya Serikali kuingilia kati, lakini limeacha maswali mengi
Yanga ina kila sababu ya kusimamia kwenye kanuni kwani imeadhibiwa mara nyingi na TFF kwa makosa ya kutozingatia kanuni hizo
Mpaka wakati huu Makamu Mwenyekiti wa Yanga Fredrick Mwakalebela yuko kifungoni kujihusisha na masuala ya soka kwa miaka mitano ukiuliza utaambiwa kanuni..kanuni...kanuni...
Jitihada zilifanyika kumnasua kutoka kifungoni Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli ambaye naye alifungiwa miaka mitano
Hakuna timu iliyopigwa faini nyingi msimu huu kuizidi klabu ya Yanga, makosa ni yaleyale, hamfuati kanuni...
Sasa May 08 Yanga wamefuata kanuni wanaambiwa watumie busara..!
Yanga ina kesi nyingi zimekwama TFF pasipo kusikilizwa, Serikali iliagiza TFF na Yanga wakae chini 'wayamalize', lakini kwa hakika jambo hili litakuwa gumu kwani hakuna dhamira ya dhati
Uongozi wa Yanga unazo sababu za kuweka msimamo ili TFF nao waheshimu kanuni za kuendesha mashindano ya soka Tanzania
Hii ni pamoja na kusikiliza mashauri ya Yanga yaliyopo kwenye kamati zao mbalimbali