Mshambuliaji wa Yanga Princess Aisha Masaka amemaliza kinara wa kuzifumania nyavu kwenye ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite' iliyofikia tamati jana
Masaka ameibuka na kiatu cha dhahabu baada ya kuweka kambani mabao 35
Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, Injinia Hersi Said, amemkabidhi Masaka tuzo ya kiatu cha dhahabu
Injinia Hersi amesema, Masaka ameweka rekodi za kipekee kwenye ligi ya Wanawake msimu huu
1. Magoli mengi zaidi - 35
2. Magoli mengi zaidi katika mchezo mmoja - 5
3. Hat trick nyingi zaidi - 4
4. Hat trick ya haraka zaidi - dakika 15
"Nichukue fursa hii kukupongeza sana kwa mafanikio yako binafsi lakini pia kwa timu nzima chini ya kocha @ednalema_mourinho"
"Edna amekuwa ni nguzo imara katika maendeleo ya @yangasc_princess pamoja benchi lake zima la ufundi kwa uratibu wa @malza12"
"Inshallah, mwakani muanzie hapo mlipoishia kufikia malengo makubwa zaidi,"aliandika Injinia Hersi kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii