Kiungo mshambuliaji wa Yanga Saido Ntibazonkiza amewataka wanachama na mashabiki wa klabu hiyo waendelee kuwapa sapoti licha ya kukosa ushindi katika mchezo dhidi ya Namungo Fc uliopigwa Ruangwa jana
Saido ndiye aliyechonga kona iliyopelekea tukio la kukataliwa bao lililofungwa na Yacouba Songne katika mchezo uliomalizika kwa suluhu ya bila kufungana
Saido amesema wataendelea kupambana kuhakikisha wanafanya vizuri katika mchezo unaofuata dhidi ya JKT Tanzania
"Tunawashukuru wanachama, wapenzi na Mashabiki wetu kwa kujitokeza uwanja wa Majaliwa Ruangwa, Tunawashukuru sana ila hatukufanikiwa kupata alama tat"
"Tutaendelea kupambana kwenye Mchezo ujao dhidi JKT Tanzania pale Dodoma, Tunawaomba muendelee kutuunga mkono," aliandika Saido kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Yanga ilirejea mkoani Mtwara kujiandaa na mchezo dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa Jumatano, May 19 uwanja wa Jamhuri, Dodoma