Ukiachana na tukio la utata la Yanga kunyimwa bao katika mchezo dhidi ya Namungo Fc jana, bado kocha Nasreddine Nabi ana kazi ya kufanya kukiimarisha kikosi chake
Bado changamoto kwenye eneo la ushambuliaji ipo, timu haiwezi kupata ushindi bila ya kufunga mabao
Katika viwanja vigumu kama kile cha Majaliwa, ni muhimu sana kwa wachezaji kutumia nafasi chache wanazopata
Ni wazi mwendelezo wa matokeo haya ya sare sare yanafifisha matumaini ya Yanga katika mbio za ubingwa
Kwa mechi zilizobaki ni vyema 'focus' ikabaki kwenye kupata matokeo chanya kuliko kufikiria sana ubingwa
Kwani presha imeanza kuongezeka hata katika nafasi ya pili, Azam Fc wameendelea kufanya vizuri wakati Yanga inasuasua
Ushindi wa mabao 2-1 waliopata jana dhidi ya KMC umewafanya Azam Fc wafikishe alama 57, sasa wakitofautiana na Yanga kwa alama moja tu pamoja na kuwa Azam Fc wamecheza mechi moja zaidi
Ni mwezi uliopita tu Yanga ilikuwa mbele ya Azam Fc kwa alama tisa, lakini sasa imebaki alama moja
Yanga inahitaji kushiriki michuano ya ligi ya mabingwa msimu ujao, kupata nafasi hiyo ni lazima washinde ubingwa au wamalize katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom