Kikosi cha Yanga kimepania kuanza vyema michuano ya Kombe la FA, wakati itakapomenyana na Reha FC, kwenye uwanja wa Uhuru kesho Jumapili.
Kocha msaidizi Shedrack Nsajigwa, amesema maandalizi yanakwenda vizuri na anafurahia kurejea kwa baadhi ya wachezaji nyota waliokuwa majeruhi ambao baadhi yao amepanga kuwaanzisha kwenye mechi hiyo.
"Tunaendelea vizuri na mazoezi na mpaka sasa wachezaji wote wapo fiti na wanafanya mazoezi ispokuwa Feston Kayembe, ambaye alikwenda kwao Kongo, lakini hajarudi lakini waliobaki wote wapo sawa,"amesema Nsajigwa.
Nsajigwa ambaye ni nahodha wa zamani wa timu hiyo amesema anachotaka ni kuanza vizuri kwa kupata ushindi mnono kwenye mchezo huo ambao kwao ni wa ufunguzi katika mzunguko wa pili wa michuano hiyo.
Amesema baada ya kutolewa katika hatua ya nusu fainali mwaka jana mwaka huu wanataka kulirudisha kombe lao na tayari wameanza harakati za kuhakikisha wanashinda kila mchezo ambao wanacheza hivi sasa.
Yanga imepata 'mzuka' wa kuhakikisha inaiondosha Reha FC kwenye michuano hiyo ili kuepuka kilichowakuta Simba jana

ADVERTISE HERE