Mshauri wa Yanga Senzo Mazingisa amesema mabingwa hao wa kihistoria walijipanga kuwakabili watani zao Simba, walikuwa tayari kuwapa furaha mashabiki wao
Senzo amesema hawakufurahishwa na kile kilichotokea kupelekea mchezo huo kushindwa kufanyika, wanasubiri maamuzi yatakayofikiwa na wenye mamlaka ya usimamizi wa soka nchini
Aidha Senzo amesema yapo mabadiliko ya kiuchezaji kikosi cha Yanga kinaonyesha sasa tangu ujio wa kocha mpya Nasreddine Nabi
"Timu yetu imeanza kuimarika sana, ni bahati mbaya mchezo wa Simba uliahirishwa, lakini wanachama na mashabiki wangeona kitu tofauti, wachezaji wameanza kumuelewa kocha kwa kiasi kikubwa," alisema Senzo
Senzo ameongeza kuwa kwa sasa mawazo yao yote ni kuelekea mchezo dhidi ya Nambungo Fc ambao utapigwa Jumamosi, May 15 katika uwanja wa Majaliwa, Lindi
"Mchezo hautakuwa mwepesi, lakini kwa sasa tuna kikosi ambacho ukiongeza mbinu za Mwalimu, mashabiki watarajie kuona kitu tofauti hasa kuongezeka kwa ubora wa mbinu"