Wananchi wamesikia mengi lakini, jambo moja bado, tamko la kubadili muda wa mchezo kutoka saa 11 jioni kwenda saa moja usiku lilitolewa na nani?
Mpaka sasa sio TFF, wala Bodi ya Ligi iliyobainisha nini sababu ya mchezo huo kupelekwa mbele zaidi ya kuitaja Serikali
Serikali inayotajwa kutoa agizo hilo, kupitia kauli ya Waziri Mkuu mapema leo, hata wao wanasikitika na wameiagiza Wizara na TFF kutoa maelezo ya nini kilitokea pamoja na mashabiki kuambiwa mustakabali wa fedha zao pamoja na kujua hatma ya mchezo huo
Hata Simba ambao kupitia tamko lao walipendekeza Yanga ishushwe madaraja mawili kwa kukaidi agizo la Serikali, hawajataja agizo hilo
kwa ufupi hakuna mwenye majibu amri ilitolewa na nani huko Serikalini?
Leo Kamati ya saa 72 ilikutana kujadili mchezo huo, je majibu ya maswali hayo yatapatikana? au wataongeza maswali zaidi? tusubiri..!
Lakini Wananchi hawana presha yoyote kwani wao wamesimama kwenye upande wa haki