Mansour ni shabiki kindaki ndaki wa Yanga kutoka kule mkoani Kigoma ambeya amefanya tukio la kihistoria ambalo linapaswa kuingizwa katika vitabu vya kumbukumbu
Shabiki huyu ametembea kwa mguu kutoka mkoani Kigoma mpaka jijini Dar es salaam kuja kushuhudia mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga uliokuwa upigwe juzi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Hata hivyo ilikuwa bahati lengo lake la kushuhudia mchezo huo halikufanikiwa kwani uliahirishwa baada ya mkanganyika na mabadiliko ya muda yaliyofanywa na TFF saa chache kabla ya mchezo kupigwa

Lakini kama ilivyo ada, Yanga imetambua thamani ya kile kilichofanywa na Mansour, amekaribishwa Makao Makuu kuonana na viongozi
Amefanya tukio kubwa ambalo limestahili kutambuliwa na klabu na pengine anastahili kupewa shukrani ya kipekee
Ni kawaida kwa mashabiki wa soka kutoka mikoa mbalimbali kuja jijini Dar es salaam kushuhudia timu yao inapocheza na Simba
Msimu uliopita mashabiki watatu walitokea mkoani Mtwara kwa baiskeli kuja jijini Dar es salaam kushuhudia mchezo dhidi ya Simba