Baada ya mchezo dhidi ya Simba kuahirishwa, Wananchi watasafiri kuelekea mkoani Lindi ambako wanakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Namungo Fc ambao utapigwa Jumamosi, May 15, 2021
Mchezo utachezwa Wilayani Ruangwa katika uwanja wa Majaliwa kuanzia saa kumi kamili Alasiri
Huo utakuwa mchezo wa duru ya pili baina ya timu hizo baada ya mchezo wa kwanza uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa kumalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Wakati Yanga wakimalizana na Namungo, watani zao Simba hawajacheza mchezo wowote dhidi ya Namungo msimu huu sababu ikielezwa ni ushiriki wa timu hizo kwenye michuano ya CAF
Kikosi cha kocha Nasreddine Nabi kinazihitaji alama zote tatu kutoka mchezo huu ili kuhakikisha wanaendelea kubaki kwenye mbio za kuwania ubingwa msimu huu