Yanga Princess imeweza kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya JKT Queens katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite' ambao ulipigwa uwanja wa Uhuru
Mchezo huo uliopigwa saa nane mchana, uliishuhudia Yanga Princess ikifunga mabao yake kupitia kwa Aisha Masaka na Amina Ally
Masaka amefikisha mabao 28 sasa ndiye kinara wa mabao katika ligi kuu ya Wanawake
Ushindi huo umeifanya Yanga Princess ifikishe alama 47 alama moja nyuma ya Simba Queens inayoongoza ligi ikiwa na alama 48
Timu zote zimebakisha michezo minne kumaliza msimu
ADVERTISE HERE