Sanga atangaza Kamati ya Mabadiliko Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
22 Dec 2017
Sanga atangaza Kamati ya Mabadiliko Yanga
Kaimu Mwenyekiti wa Yanga Clement Sanga leo ametangaza majina ya wajumbe wa Kamati iliyoundwa kupendekeza/kushauri mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ya Yanga.

Akizungumza na waandishi wa Habari Makao Makuu ya klabu ya Yanga jijini Dar es salaam leo, Sanga amesema Kamati hiyo imeundwa na wataalamu waliobobea katika nyanja mbalimbali.

Kamati hiyo yenye Wajumbe sita itaongozwa na Mwenyekiti Alex Mgongolwa ambaye kwa taaluma yake ni Mwanasheria.

Wajumbe wa Kamati hiyo ni pamoja na Prof Gamaliel Mgongo Fimbo, mtaalamu wa masuala ya Katiba na Sheria za Ardhi, Said Mecky Sadik aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na baadae Kilimanjaro.

Wengine ni George Fumbuka, mshauri wa masuala ya uwekezaji, Felix Mlaki, mchumi na mtaalamu wa masuala ya fedha.

Pia yumo Mohammed Nyenge, ambaye kitaaluma ni mchumi lakini pia akiwa Mwenyekiti wa Kamati ya uchumi na Mipango ya klabu ya Yanga.

Kamati hiyo itapendekeza mfumo wa mabadiliko ya uendeshaji wa klabu ya Yanga.

Baada ya kupokea mapendekezo hayo, Kamati ya Utendaji wa Yanga itaanza rasmi mchakato wa mabadiliko kwa kutoa elimu kwa Wanachama kisha kuitisha Mkutano Mkuu utakaopitisha mfumo huo mpya utakaokuwa umependekezwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
5h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
10h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
10h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
20h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
23h ago
READ MORE β†’