Mchezo dhidi ya Simba uliokuwa upigwe leo uwanja wa Benjamin Mkapa umeahirishwa
Hata hivyo Yanga ilifuata taratibu zote za mchezo wakifika uwanjani mapema na kuingia uwanjani ilipofika saa 11 muda uliokuwa umepangwa mchezo huo kupigwa
Yanga ilisubiri kwa dakika 15 lakini watani zao Simba hawakutokea uwanjani
Kimsingi Yanga inastahili kupewa alama 3 kwa makosa yaliyofanywa na Simba kwa kushindwa kutokea uwanjani ndani ya muda wa mchezo
Aidha taarifa iliyotolewa mapema na TFF kubadili muda wa mchezo huo ni kinyume na kanuni kwani walipaswa kuzitaarifu timu zote saa 24 kabla ya mchezo
Hata hivyo ni wazi mchezo huo utapangiwa tarehe nyingine tu bila wahusika waliosababisha kadhia hii kuchukuliwa hatua
Lakini Yanga wanayo haki ya kudai alama tatu kwa kuwa mpinzani wake Simba hakutokea uwanjani katika muda uliokuwa umepangwa awali kwa mujibu wa kanuni