Yanga imetimiza ahadi yake kwa kusisitiza mchezo dhidi ya Simba ulipaswa kupigwa saa 11 jioni kama ulivyopangwa awali kwa kuwa mabadiliko yaliyofanyika leo yako nje ya kanuni ya uendeshaji wa mpira wa miguu iliyotungwa na Bodi ya Ligi/TFF wenyewe
Yanga ilifika uwanjani mapema, wachezaji wakafanya mazoezi kwa takribani dakika 20 kisha wakaingia uwanjani kusubiri muda wa mchezo
Baada ya dakika 15 Yanga imeondoka uwanjani
Ni jukumu la wasimamizi wa soka Tanzania kuhakikisha wanafuata kanuni na taratibu walizozitunga wao wenyewe
Yanga imefanya kitu sahihi kwa kufuata taratibu kama zinavyoelekeza
ADVERTISE HERE