Ni dabi day, mechi ya kufa au kupona

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
8 May 2021
Ni dabi day, mechi ya kufa au kupona

Mabingwa wa kihistoria Tanzania Yanga leo majira ya saa 11 jioni watashuka katika uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili wapinzani wao Simba katika mchezo wa dabi, ligi kuu ya Vodacom

Ni mchezo ambao utasimamisha nchi kwa takribani masaa mawili kwa miamba hao wa soka kuonyeshana kazi ndani ya dimba la Mkapa

Kwa Yanga huu ni mchezo muhimu kupata ushindi ili kuendelea kubaki katika mbio za kuwania ubingwa wa VPL msimu huu

Yanga iko nyuma kwa tofauti ya alama nne dhidi ya watani zao Simba ambao wanaongoza ligi wakiwa na alama 61

Pia utakuwa mchezo wa kwanza wa dabi kwa kocha Mohammed Nasreddine Al Nabi aliyetua Yanga mwezi uliopita kuchukua mikoba ya Cedric Kaze

Ni dabi ya Kariakoo, mechi ambayo kitakachofanyika ndani ya dakika 90 kinaweza kuwa na athari hasi au chanya kwa timu na hata mchezaji mmoja mmoja

Pamoja kuvuna sifa na kuilinda heshima ya Yanga, kama wachezaji watajitoa leo na kuondoka na ushindi, watatoa ujumbe kwa watani zao kuwa wanaweza kumfunga yeyote nje ya Tanzania, lakini hapa ndani mfalme ni mmoja tu, Yanga

Ni mchezo ambao wachezaji watajaa 'mapesa' kama watafanikiwa kuwapa furaha mabosi wao ambao wameweka mezani ahadi kubwa ya fedha kwa ajili yao

Huu ni mchezo wa heshima, mechi ambayo inaweza kuipandisha au kuishusha thamani ya mchezaji

Wapinzani wao Simba kupitia msemaji wao, wamekuwa wakitamba kila kona, wanajitapa kuwa watashinda huku wakiwabeza wachezaji wa Yanga

Dharau, kashfa na kebehi wanaweza kuzijibu leo kwa kuhakikisha wanakwenda 'kuwalaza na viatu' mapema

Yanga haijawahi kushindwa inapokuwa na jambo lake, kwa hakika leo pia hawatashindwa kuwapa furaha mashabiki wao pale kwa Mkapa

Sapoti ya mashabiki pia ni muhimu sana , Afisa Mhamasishaji wa Yanga Antonio Nugaz amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi wakiwa kifua mbele na kutamba kwani leo wanapeleka kilio Msimbazi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6m ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
9h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
14h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
18h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
19h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
19h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
20h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’