Mshambuliaji wa zamani wa Yanga, Sekilojo Chambua amesema washambuliaji wa Yanga wanapaswa kuhakikisha wanafunga bao mapema ili kuwaweka katika presha Simba na kujiongezea nafasi ya kushinda mchezo huo
Chambua amesema kwa uzoefu alionao na michezo hiyo ya dabi, timu inayofunga bao mapema inakuwa nafasi nzuri zaidi ya kushinda kwani wapinzani watakuwa katika presha kubwa baada ya kuruhusu bao
"Mastraika wa Yanga ndio wanajukumu la kuiua Simba, wanatakiwa kuwa makini na watulivu kwenye kila nafasi ya kufunga watakayoipata ili kuitumia vyema na kufunga."
"Wakiweza kutangulia kufunga itawapa nguvu Yanga kwani Simba licha ya kuwa na wachezaji wengi bora lakini wataanza kucheza kwa presha kubwa jambo ambalo litawafanya wakose maelewano mazuri"
"Wote tumecheza mpira hivyo presha ya kutangulia kufungwa tena kwenye mechi kubwa kama hiyo tunaijua, hivyo basi utulivu wa hali ya juu, kujiamini na kujitoa kwaajili ya timu kwa washambuliaji na wachezaji wengine wa Yanga ndivyo vitawafanya kuibuka na ushindi katika mechi ya Jumamosi," alisema Chambua