Tuko tayari kuwakabili, hatuwaogopi - Nabi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 May 2021
Tuko tayari kuwakabili, hatuwaogopi - Nabi

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa dabi dhidi ya Simba ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Akizungumza katika kikao na Wanahabari leo, Nabi amesema mchezo kati ya Simba na Yanga, ni moja ya mechi kubwa za dabi hapa Afrika

Amesema anafahamu anakwenda kukutana na Simba ambayo iko katika kiwango bora wakipata mafanikio kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Hata hivyo pamoja na kuwaheshimu Simba, Nabi amesema wamejiandaa kikamilifu kupambana nao na kuwa hawaogopi

"Simba ni timu nzuri lakini ina mapungufu yake, tunaiheshimu lakini hatuihofii. Maandalizi ya mechi ni yale yale kama ya michezo mingine tofauti ni uchezaji"

"Tunajua mchezo utakuwa mgumu lakini tumejiandaa kushinda," alisema Nabi

Naye Haruna Niyonzima aliyeambatana na Nabi katika Mkutano huo, amesema wachezaji wamejiandaa kupambana kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo huo

Amesema ni mchezo mkubwa ambao unahitaji wachezaji wakubwa, mchezo huo utatoa nafasi kwa wachezaji kudhihirisha kuwa hawakusajiliwa Yanga kwa bahati mbaya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
7h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
10h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
22h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’