Kiungo Carlos Carlinhos hatakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoikabili Simba siku ya kesho katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom
Juzi Carlinhos alifanyiwa vipimo vya majeraha aliyopata mkoani Rukwa katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons ambapo imebainika kuwa nyota huyo kutoka Angola amechanika nyama za paja
Carlinhos atakuwa nje kwa takribani wiki mbili kuuguza majeraha hayo
Aidha, uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa mlinzi wa kushoto Yassin Mustafa nae atakosekana siku ya Jumamosi akiuguza majeraha

Yassin nae atarejea uwanjani baada ya wiki mbili
Upande wa kushoto kocha Nasreddine Nabi anatarajiwa kumtumia Adeyum Saleh ambaye amecheza mechi tatu zilizopita wakati Fei Toto atarejea kuchukua nafasi ya Carlinhos
ADVERTISE HERE