Hii Yanga inajengwa Kimataifa aisee

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2021
Hii Yanga inajengwa Kimataifa aisee

Hebu angalia sifa za watu hawa ambao wamepewa jukumu la kuliongoza benchi la ufundi la Yanga

NASREDDINE Mohamed Nabi, Mtunisia na Mbelgiji, aliyeweka makazi kwa muda mrefu Mkoani Blauwnberg, nchini Ubelgiji ni Mwalimu mwenye hadhi ya juu aliye na leseni ya UEFA Pro huku akiwa na uzoefu wa kutosha wa Soka la Afrika kwa takribani miaka 16, analijua nje ndani, hata yale mambo "yao" ya kuingia Uwanjani usiku bila woga, anayajua

Wakati Chipolopolo inachukua Ubingwa wa Afrika wa Kumfunga Ivory Coast kwa Penalty, jina la Herve Renald, Kocha wa Klabu bingwa Afrika kwa mara ya saba Al Ahly, Hossam El Badry, Nabir Maaloul (Esperance) na mtaaluma Nasreddine Nabi (AC Leopard) yaliwekwa pamoja katika kumtafuta Kocha Bora wa Afrika, unaweza kuona ni Nabi pekee ambaye ametoka katika timu ya "kawaida".

Mwalimu toka El Merreikh, AC Leopards, Ismaily, Al Hilal na Darling Club Motema Pembe, huku kote amefanikiwa kupata makombe zaidi ya sita, katika nchi tofauti za Afrika;

Unahitaji Mwalimu kama huyu ili uweze kutengeneza timu iliyobora, Mwalimu ambaye ameshashiriki kuanzisha au kuendeleza timu zenye mashabiki "vichaa" wa Soka barani Afrika

Mwalimu mwenye Msimamo ambaye anaweza kusimama na kufanya maamuzi magumu kwa manufaa ya Klabu

Usichojua, Nabi ni mpenzi mkubwa wa "possession football", pasi fupi, za haraka na kwenda mbele, ni muumini mkubwa wa mfumo wa 4-1-4-1 ambayo huwa mara nyingi anaigeuza kwenda 4-5-1, 4-2-3-1, 5-4-1,3-4-3, ila pia yuko "very flexible" kama ukiangalia timu zake za awali zinavyocheza

JAWAD Sabri, mmoja kati ya walimu bora kabisa Afrika katika "Physical and Fitness".

Mwalimu huyu wa Kimorocco, ni Daktari wa PhD, aliyetokea katika Klabu ya Raja Casablanca na amekuwa akishirikiana na chama cha Soka Morocco kwa timu zao zote za Taifa

Yanga SC imevunja mkataba wa Mwalimu huyu na Raja ili aje kuhudumu Tanzania, hii inakupa picha ya Klabu katika kutawala Soka la Afrika hivi karibuni.

SGHIR Hammadi ni Mbelgiji ambaye ni Mwalimu wa mpira mwenye leseni A ya UEFA, lakini pia kwa sasa ndiye mtaaluma nambari moja Tanzania kwenye Soka la Vijana maana ndiyo Mwalimu PEKEE mwenye leseni ya UEFA A mahususi kwa Vijana

Huyu anauwezo mkubwa sana wa kututengenezea mtaala ambao utatumika kuanzia Yanga U17&20 mpaka juu

RAZACK Siwa, mmoja kati ya walimu bora kabisa wa magolikipa Afrika ya Mashariki, uzoefu wake umewafanya magolikipa wengi sana kuuzwa na wengine kurudi na kuhudumu vyema timu zao za Taifa

Razack anakibarua kingine cha kuhakikisha Farouk Shikhalo, Metacha Mnata, Ramadhan Kabwili, Geofrey Magaigwa, Aziz Junior na wengine wa U17&20 wanakua katika ubora wa hali ya juu kwa faida ya Klabu yetu na Taifa kwa ujumla

FARIED Cassiem, Physio kutoka Afrika ya Kusini ambaye uwezo wake katika maswala haya ni mkubwa na ni mtu ambaye anaendelea kuwafunza vijana wengine wa Kitanzania katika kuwarithisha taaluma kubwa mno aliyonayo kwa faida ya nchi

Dr SHEIKH Mngazija, huyu ni mmoja ya madaktari wasiozidi watano Tanzania wenye uzoefu kama wake katika medani ya michezo.

Ameshahudumu Timu ya Taifa Tangu Awamu ya Mwinyi, Mngazija anapaswa kupewa maua yake angali yuko hai, ni mmoja kati ya watabibu waliojitoa haswa katika tasnia ya michezo nasi tukiwa tunajiandaa kuichukua Afrika

HAFIDH Saleh ndiyo Manager wa Timu mzoefu haswa na Soka la Tanzania na Afrika, anajua mambo muhimu sana ya Soka letu na kipi kifanyike ili tuendelee kuwa pamoja

Kwako MwanaYanga, Ukiona hili Benchi la Ufundi, tambua kuwa Klabu kupitia kwa mfadhili GSM imewekeza kwa vitendo na Malengo ni makubwa kuliko sauti za hao wapinzani

Iamini timu yako, liamini benchi la Ufundi, acha wafanye kazi nasi tusubiri matunda

Credit : Babaparoko

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
10h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
14h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
15h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
15h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’