Mzee Mpili atinga Jangwani

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2021
Mzee Mpili atinga Jangwani

Disemba 14, 2019 Yanga ilimpoteza moja ya wapambanaji wake, Mzee Ibrahim Akilimali aliyefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mrefu

Hakuna Mwanayanga ambaye hakumfahamu Mzee Akilimali enzi za uhai wake

Hakuogopa kuzungumza pale alipoona mambo hayaendi sawa. Wakati mwingine aliingia kwenye mgogoro na Wanachama wenzake kutokana na msimamo mkali aliokuwa nao

Wazee hawa wana umuhimu wao katika vilabu vyetu hivi kwani wao ndio wamekuwa navyo na wanafahamu mambo ya ndani zaidi

Katika mitandao ya kijamii bila shaka umewahi kukutana na vipande vya video za Mzee Mpili kutoka kule Ikwiriri, Rufiji

Mzee huyu amejipambanua kuwa Mwanayanga kwelikweli, mara kadhaa amesikika akiwaonya wale waliojaribu kuivuruga Yanga hasa baada ya GSM kuingia kuweka mambo sawa

Mzee Mpili leo alipata nafasi ya kufika Makao Makuu ya klabu ya Yanga, akapokewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Hassan Bumbuli

Kuelekea mchezo wa Jumamosi dhidi ya Simba, Wazee hawa sio wa kuwapuuza! kwani wanafahamu mambo mengi hasa zinapokuja mechi hizi za dabi!

"Ukiwa kiongozi ni muhimu Sana kuwasikiliza wale unaowaongoza wanasemaje? Wanashauri nini na wana maoni gani? Leo nimekutana na Mzee Mpili, moja ya Wanachama na Wazee mashuhuri wa Yanga kutoka Rufiji," aliandika Bumbuli katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’