Feisal Salum 'Fei Toto' mechi yake imewadia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 May 2021
Feisal Salum 'Fei Toto' mechi yake imewadia

Jumamosi hii Wananchi watashuka pale uwanja wa Benjamin Mkapa kuwakabili watani zao Simba katika mchezo wa kukata na shoka, ligi kuu ya Vodacom

Ni mchezo ambao Yanga itakuwa na kazi moja tu, kuhakikisha inaondoka na alama zote tatu ili kurejesha matumaini ya kuwania ubingwa msimu huu

Ukitaja mchezo wa watani wa jadi, huwezi kukosa kutaja jina la kiungo Feisal Salum 'Fei Toto' fundi mmoja kutoka kule visiwani Zanzibar

Fei Toto ameshiriki mechi karibu zote za dabi tangu alipojiunga na Yanga misimu mitatu iliyopita

Michezo hii yenye presha ndio humpaisha Fei Toto kwani huwa anaimudu sana

Katika mchezo wa duru ya kwanza, yeye na Mukoko Tonombe 'walikichafua' kwelikweli katika eneo la kiungo, Mukoko akiondoka na tuzo ya nyota wa mchezo

Fei Toto anapokuwa uwanjani katika mchezo wa dabi, yule kiungo wao Mzambia wanaomsifia sana huwa haonekani!

Ataonekana vipi mbele ya Mzanzibar huyu ambaye kipaji chake ni cha asili!

Fei Toto amepona majeraha yaliyomuweka nje kwa mechi kadhaa. Amepata mapumziko muhimu baada ya kutumika kwa muda mrefu

Jumamosi hii anatarajiwa kurejea pale kwa Mkapa kuwakabili Simba, mechi ambayo kwake ni swa na 'kumsukuma mlevi'

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
9h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
13h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
18h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
18h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’