Katika michezo ya nyuma tumeshuhudia waamuzi sita wakichezesha mchezo wa watani wa jadi kati ya Yanga dhidi ya Simba
Lakini kwenye mchezo wa Jumamosi waamuzi watakuwa wanne tu kama ilivyo katika michezo mingine
Mwenyekiti wa kamati ya waamuzi, Soud Abdi ametolea ufafanuzi wa Mabadiliko hayo ambayo kimsingi yamesababishwa na Mabadiliko ya kiufundishaji yaliyofanywa na Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF)
Soudi amesema waamuzi wa kati wamepewa majukumu ya ziada yaliyokuwa yakifanywa na waamuzi waliokuwa wakisimama nje ya kila goli. CAF ilitoa mafunzo kwa waamuzi kuhusu mabadiliko hayo
"Safari hii tumeweka waamuzi wanne na si sita kama ilivyozoeleka hasa linapokuja suala la mechi za aina hii, kwasababu CAF wametoa muongozo kwamba kuanzia sasa majukumu yaliyokuwa yanafanywa na mwamuzi wa ziada, sasa yatafanywa na mwamuzi wa kati mwenyewe," alisema Soud
Ufafanuzi huo unaelezo kuwa, mwamuzi wa kati atalazimika kusimama kwenye kona ya nje ya mstari wa eneo la 18 kushoto kama mchezo utakuwa ndani 18, huku akilazimika kusimama nje ya mstari wa 18 ya mpinzani akiwa nusu usawa wa kati na usawa wa goli.
Maelezo hayo pia, yamelenga kumuongezea ujuzi mwamuzi wa kati ili imsaidie kuongeza ufanisi wa maamuzi yake
Waamuzi waliochaguliwa kuchezesha mchezo Jumamosi ni, Mwamuzi wa kati, Emmanuel Mwandembwa, waamuzi wasaidizi ni Frank Komba na Hamdani Saidi na mwamuzi bora wa msimu uliopita, Ramadhani Kayoko kuwa mwamuzi wa akiba