Kuelekea mchezo wa watani wa jadi ambao utapigwa Jumamosi May 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa, mlinzi wa kulia wa Yanga Kibwana Shomari ataingia katika mchezo huo akiwa na rekodi ya kipekee
Katika wachezaji wote wa Yanga na Simba, Kibwana ndiye anayeshikilia rekodi ya kucheza dakika nyingi
Kibwana amecheza jumla ya dakika 2137 ambazo ni sawa na takribani michezo 24
Kinda huyo aliyetua Yanga kutoka Mtibwa Sugar, amekuwa na msimu mzuri ndani ya kikosi cha Yanga
Ni mchezaji tegemeo katika safu ya ulinzi ya Yanga upande wa kulia
Ameshiriki mechi zote mbili dhidi ya Simba msimu huu, mchezo wa Jumamosi unatarajiwa kuwa wa tatu
ADVERTISE HERE