Mkifungwa na Yanga kubalini matokeo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 May 2021
Mkifungwa na Yanga kubalini matokeo

Naibu Waziri wa Utumishi na Utawala Bora Deogratius Ndejembi amezitaka timu zinazofungwa na Yanga kukubali matokeo badala ya kutoa visingizio vya kuhongwa

Ndejembi ametoa kauli hiyo siku chache baada ya kauli ya nahodha wa Tanzania Prisons Benjamin Asukile ambaye aliituhumu Yanga kutoa hongo ya Tsh Milioni 40 katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Wajelajela hao, mchezo ambao ulimalizika kwa Yanga kushinda bao 1-0

Yanga ilimtaka Asukile athibitishe tuhuma zake na wakati huohuo ikichukua hatua kwa kumfikisha kwenye vyombo husika aweze kuchukuliwa hatua

Ndejembi amesema Yanga ni miongoni mwa timu bora na zenye historia kubwa barani Afrika, hivyo ni jambo la ajabu timu kudai kuhujumiwa pale zinapofungwa na Yanga

"Kumekuwa kuna tabia ya viongozi wa timu hapa nchini hasa wakifungwa na Yanga kihalali hutoa kauli kwamba wamehongwa, ifike wakati wakubali wanapofungwa wakubaliane na matokeo," alisema 

Katika hatua nyingine,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Innocent Bashungwa amesema Serikali haitofumbia macho wanaotumia rushwa kujipatia ushindi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’