May 08 'kitaeleweka' kwa Mkapa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 May 2021
May 08 'kitaeleweka' kwa Mkapa

Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi anakiandaa kikosi chake kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, May 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Hii itakuwa mara ya pili Nabi anawakabili Simba katika mwaka huu kwani aliiongoza Al Merrikh katika mchezo wa ligi ya mabingwa uliopigwa Sudan ambao ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana. Nabi aliachana na Al Merrikh baada ya mchezo huoΒ 

Baada ya kuivusha Yanga hatua ya robo fainali michuano ya kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) kwa ushindi wa ugenini dhidi ya Tanzania Prisons, Nabi amesema matokeo hayo yamekiongezea kikosi chake morali kuelekea mchezo dhidi ya Simba

Aidha kocha huyo raia wa Tunisia amesisitiza kuwa hawatakuwa tayari kupoteza mechi mbili mfululizo katika ligi baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Azam Fc

"Simba inafanya vizuri katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania bara, lakini hilo halituzuii kufanya vema katika mchezo dhidi yao Jumamosi na kuondoka na pointi tatu"

"Baada ya kupata matokeo na kuingia hatua ya nane bora tunarudi kutafuta pointi tatu, najua utakuwa mchezo mgumu kwa upande wetu lakini naamini tunaenda kupata ushindi na kuondoka na pointi tatu, " alisema Nabi

"Naiheshimu Simba ni timu nzuri yenye wachezaji wazuri lakini kwa maandalizi tunayofanya, naamini tunaenda kuchukua pointi tatu na kupunguza idadi ya pointi walizotuzidi"

Mchezo wa Jumapili utakuwa wa pili kuzikutanisha timu hizo msimu huu katika michuano yote

Mchezo wa kwanza ni ule wa ligi kuu duru ya kwanza ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Watani hao wa jadi wakakutana tena visiwani Zanzibar kwenye mchezo wa fainali michuano ya kombe la Mapinduzi, Yanga ikiibuka washindi kwa mikwaju ya penati baada ya mchezo kumalizika kwa suluhu ya bila kufungana

Takwimu za kuanzia msimu uliopita, Yanga imepoteza mchezo mmoja tu dhidi ya Simba (ASFC) katika michezo mitano waliyocheza.

Wameshinda mechi mbili na kutoka sare miwili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’