Kikosi cha Yanga kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi, May 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema baadhi ya wachezaji majeruhi na wale waliopata changamoto za hapa na pale katika mchezo uliopita wanaendelea vizuri
Dickson Job, Metacha Mnata na nahodha Lamine Moro ni miongoni mwa wachezaji hao huku kiungo Carlos Carlinhos akifanyiwa vipimo Hospitalini majibu yake yakitarajiwa kutolewa Jumanne
Habari njema ni kurejea kikosini Tuisila Kisinda ambaye madaktari wamemruhusu kufanya mazoezi na wenzake licha ya kuwa atafanyiwa vipimo zaidi kubaini utimamu wake
Bumbuli amewahakikishia mashabiki wa Yanga kuwa kikosi chao kiko imara na kinaendelea vyema na maandalizi kuelekea mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla