Nawakumbusha tu, TK Master atakuwepo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 May 2021
Nawakumbusha tu, TK Master atakuwepo

Winga machachari wa Yanga Tuisila Kisinda alipata majeraha katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Gwambina Fc na kupelekea akakosa michezo miwili iliyofuata dhidi ya Azam Fc na Tanzania Prisons

Habari njema ni kuwa Kisinda sasa yuko timamu kwa asilimia 100 kuelekea mchezo dhidi ya Simba utakaopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa Jumamosi

Ndio! siku hiyo Kisinda ataendeleza pale alipoishia katika mchezo wa duru ya kwanza ambao ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1

Kisinda aliwapa wakati mgumu walinzi wa Simba katika mchezo huo na hata ule wa kombe la Mapinduzi ambao ulipigwa visiwani Zanzibar

Kwa hakika hautakuwa mchezo mwepesi kama wanavyodhani kwani pamoja na Kisinda, lakini pia safu ya ushambuliaji ya Yanga itakuwa na wachezaji kama Michael Sarpong, Saido Ntibazonkiza, Carlinhos akitarajiwa kuongezeka katika eneo la kiungo huku Yacouba Songne akiwa 'amenogewa' kufunga

Yacouba yuko katika kiwango bora sana akifunga mabao matatu katika michezo minne iliyopita

Huu ni mchezo ambao Wananchi wamepania kuondoka na alama zote tatu

Β 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
21h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’