Kuelekea mchezo dhidi ya Simba ambao utapigwa Jumamosi May 08, 2021 uwanja wa Benjamin Mkapa, beki kisiki wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' amesema hana wasiwasi na kukabiliana na wachezaji wa Simba kwani anawafahamu
Ninja amecheza mechi za dabi dhidi ya Simba tangu wakati Kocha Mkuu akiwa Mwinyi Zahera na mwezi Januari katika michuano ya kombe la Mapinduzi alicheza mchezo wa fainali ambao Yanga walishinda kwa mikwaju ya penati
Ninja amedokeza ni mchezaji mmoja tu wa Simba ambaye hajawahi kukutana nae dimbani lakini anafahamu ni namna gani ataweza kukabiliana nae
"Ninatambua Simba ina wachezaji ambao ni wasumbufu ila bahati nzuri ni kwamba hao nimewahi kukutana nao uwanjani na ninajua mbinu zao"
"Labda mmoja bado ambaye ni Luis, lakini naye pia ninajua namna anavyocheza hivyo ni suala la kuomba uzima ili kila kitu kiwe sawa," alisema Ninja
Ukiacha mchezo wa kombe la Mapinduzi, mechi za nyuma Ninja alikuwa akitumika kama kiungo mkabaji katika michezo dhidi ya Simba
Ni mmoja wa wachezaji ndani ya kikosi cha Nasreddine Nabi ambao wamecheza angalau michezo miatu ya dabi dhidi ya Simba