Prisons waliingia na matokeo mfukoni

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
1 May 2021
Prisons waliingia na matokeo mfukoni

Kabla ya mchezo wa hatua ya 16 bora kati ya Prisons dhidi ya Yanga uliopigwa Sumbawanga jana na Yanga kushinda bao 1-0, Prisons waliamini wangeshinda mchezo huo

Tambo za kocha wao Msaidizi na hata wachezaji wao walizianza mapema hata kabla ya mchezo wenyewe

Prisons waliichukulia Yanga kawaida wakiamini wao wana kikosi kizuri kulikio Yanga

Aidha sare waliyopata katika michezo miwili ya ligi, iliwazidishia kiburi wakidhani Yanga ni timu rahisi sana

Lakini walipoingia uwanjani mambo yakawa tofauti. Hakukuwa na mpira wowote wa kimbinu ambao Prisons walicheza zaidi ya kubutua mbele na kuwavaa wachezaji wa Yanga kama vile ulikuwa mchezo wa rugby

Yanga hawakuwa wanyonge, walipambana na ushindi waliopata waliutafuta kwa nguvu zao

Prisons wakaishia kulilia mkwaju wa penati katika tukio ambalo lilikuwa 50-50

Nahodha wao Benjamin Asukile anaenda mbali zaidi kwa kutoa tuhuma ambazo zinaweza kumuweka matatani kama ataamriwa azithibitishe na mamlaka za soka

Lakini pia Asukile anafanya kazi ndani ya taasisi ya Jeshi, ameliaibisha Jeshi la Magereza na pengine anaweza kuchukuliwa hatua huko

Sababu ilikuwa wajibu wake kutoa taarifa mapema za hao watu wa Yanga aliodai walikuwa wakipiga simu watoe Mil 40 ili wakamatwe

Kila mmoja aliishuhudia mchezo, ukiondoa malalamiko ya kunyimwa penati, Prisons hawana cha kujivunia katika mchezo huo kwani walizidiwa na vijana wa kocha Nasreddine Nabi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
29m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
9h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’