Mlinda lango Metacha Mnata huenda leo akapata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza katika mchezo wa kombe la FA dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga
Metacha hajaonekana kikosini katika michezo ya hivi karibuni baada ya kupata msiba wa kufiwa na mtoto wake
Mlinda lango huyo aliyekuwa tegemeo kwenye duru ya kwanza VPL, sasa yuko tayari kurejea katika majukumu yake
Aidha, uongozi wa Yanga unatajwa kuwa mbioni kumuongeza mkataba, mazungumzo ya mkataba mpya yakiwa yameanza
Mkataba wa Metacha unamalizika mwishoni mwa msimu
ADVERTISE HERE