Kesho Wananchi wana jambo lao mkoani Rukwa ambapo watashuka uwanja wa Nelson Mandela kuikabili Tanzania Prisons ukiwa ni mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la FA
Yanga itaikabili Prisons bila ya wachezaji wake muhimu ambao wanatumikia adhabu za kadi
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataja Feisal Salum, Mukoko Tonombe na Michael Sarpong kuwa watakosekana kutokana na kutumikia adhabu za kadi
Hata hivyo Bumbuli amewahikikishia mashabiki wa Yanga kuwa kikosi chao kiko imara na wamedhamiria kushinda mchezo huo waweze kutinga robo fainali
ADVERTISE HERE