Yanga kubadili mbinu za usajili

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
29 Apr 2021
Yanga kubadili mbinu za usajili

Msimu wa 2020/21 unaelekea ukingoni ambapo tetesi za usajili kwa ajili ya msimu ujao zimeanza kushika kasi

Ni wakati ambao mengi husemwa, tetesi nyingine zikiwa na malengo ya kuwaongezea thamani wachezaji tu

Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano Yanga, amesema usajili wa safari hii watatumia utaratibu tofauti

Hersi amesema watafanya usajili makini ambapo watahakikisha michakato yote inafanyika katika usiri mkubwa

Hersi ameeleza kushangazwa na tetesi zilizokuwa zikiwahusu baadhi ya wachezaji wa Simba kutakiwa na Yanga

Amesema miongoni mwa wachezaji wanaowafuatilia, hakuna mchezaji hata mmoja kutoka klabu ya Simba

Amewataka Wanachama na Mashabiki wa Yanga kusubiri wakati utakapofika watafahamu ni maboresho gani wanakwenda kufanya

"Huo ulikuwa uvumi tu, Yanga haikuwa na mpango wa kusajili mchezaji wa aina yeyote pale Simba. Sisi Kama GSM tukitaka mchezaji hapa Tanzania hatuwezi kushindwa na hatutoshindwa. Usajili wa Bakari Mwamnyeto ni mfano"

"Katika orodha ya wachezaji ambao tunawafuatilia, hakuna mchezaji anatoka Simba. Usajili wa Yanga mwaka huu mtapata majibu tu, ni usiri mzito," alisema Hersi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2m ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
4h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
5h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
8h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
23h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’