Namungo Fc iliyokuwa ikishiriki michuano ya kombe la Shirikisho Barani Afrika (CAF CC) imekamilisha ratiba hapo jana kwa kufungwa bao 1-0 na Pyramids Fc ya Misri
Namungo waliokuwa wakishiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza, wamepoteza mechi zote sita lakini zaidi ni kuwa hawakufanikiwa kufunga bao hata moja
Jambo moja ambalo Namungo wanaweza kujivunia ni kuweza kushiriki michuano hiyo kwa mara ya kwanza na kufanikiwa kuingia makundi
Lakini kukosekana kwa uzoefu na kutokuwa na kikosi imara kumepelekea wakawe 'kichwa cha mwenzawazimu' kwani wamefungwa na kila timu kwenye hatua ya makundi iwe nyumbani au ugenini
ADVERTISE HERE