Tambwe afurahia ujio wa Ajib Yanga

Admin By Admin
•
6 Jul 2017
Tambwe afurahia ujio wa Ajib Yanga
Usajili uliofanywa na Yanga kwa kumsajili Ibrahim Ajib kutoka Simba sio kwamba umefurahiwa na mashabiki wa Yanga tu bali hata wachezaji wamefurahishwa na usajili huo.

Mpachika mabao mahiri Amissi Tambwe ni miongoni mwa wachezaji waliofurahia ujio wa Ajib Jangwani.

Akimwelezea Ajib Tambwe amesema ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu anayeweza kuuchezea mpira anavyotaka.

“Unajua mimi nimecheza na Ajibu pale Simba namjua vyema na sio kubahatisha niliposikia Yanga imemsajil unawezekana huo ukawa ndiyo usajili mkubwa hapa Yanga na hilo litapeleka kilio kikubwa Simba na wataligundua hilo atakapoanza kazi,”alisema Tambwe.



“Ajibu ana faida kubwa ambapo ni wachezaji wachache wanaojaliwa kuwa na kiwango kama chake, yeye anajua kuuchezea mpira lakini hatari zaidi uwezo wake huo anaweza kuutumia vyema kuwasumbua mabeki na kuufungua ukuta wowote wa wapinzani, mimi ninachokisubiri kwa hamu ni pasi zake za mwisho nilikuwa nafunga sana wakati nikiwa naye Simba.

“Ukiacha yote hayo Ajibu ana uwezo wa kufunga, sasa utaona umuhimu wa mtu wa namna hiyo, Simba wamepoteza mtu hatari sana ambaye kwasasa wanaweza wakaona kama ni kitu cha kawaida lakini ngoja ligi ianze ndiyo watajua maumivu yake namkaribisha sana tufanye kazi,”alisisitiza Tambwe.

Ajib amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga baada ya kuitosa Simba licha ya viongozi wa timu hiyo kuhaha kujaribu kumbakisha bila mafanikio.

Jangwani ameungana na washambuliaji mahiri Donald Ngoma, Amissi Tambwe na Obrey Chirwa.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
2h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
7h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
11h ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
12h ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
12h ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
13h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE →
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →