Kamati ya Uendeshaji wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania(TPLB),imemfungia michezo mitatu beki wa Simba Ibrahim Ame na kumtoza faini ya sh. 500,000 kwa kosa la kumzuia mwamuzi msaidizi kufanya kazi yake wakati wa mchezo wao na Gwambina ulichezwa Jumamosi iliyopita,Mwanza.
Katika taarifa iliyotumwa na Bodi ya Ligi leo ya kikao cha kamati hiyo iliyokaa jana Aprili 27, 2021 kupitia mwenyenendo wa matukio mbalimbali ya Ligi, mchezaji Bernard Morrison amepewa ONYO kwa kitendo kisicho cha kimichezo cha kumvuta mwamuzi msaidizi namba moja.
Morrison alifanya kitendo hicho katika mchezo dhidi ya Mwadui uliochezwa kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Aidha Simba imepigwa faini ya sh. 500,000 kwa kocha la mashabiki wake kurusha chupa uwanjani na kusababisha mchezo kusimama dakika tatu hadi Polisi kuingilia kati wakati timu hiyo ilipocheza na Gwambina.
Pia mwamuzi wa mchezo huo, Godfrey Msakila, ameondolewa katika ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu kutokana na kushindwa kumudu mchezo