Baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Azam Fc, Kocha Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi amepania kuwavusha Wananchi robo fainali ya kombe la FA pale watakapo-wakabili Tanzania Prisons keshokutwa Ijumaa
Yanga imeweka kambi ya muda mfupi mkoani Mbeya kujiandaa na mchezo huo ambapo kesho Alhamisi wanatarajiwa kuelekea Sumbawanga
Nabi alieleza kubaini mapungufu katika mchezo dhidi ya Azam Fc ambapo aliahidi kuyafanyia kazi kabla ya kuikabili Prisons
Kocha wa Makipa Razak Siwa amesema Nabi ameweka msisitizo katika safu yake ya ushambuliaji kuhakikisha wanatumia nafasi wanazotengeneza
Aidha kocha huyo raia wa Tunisia anapenda kuona wachezaji wake wanaweka mpira chini na sio butua butua huku akitaka kila mchezaji kushiriki katika ulinzi pale timu inapopoteza mpira
Siwa amesema benchi la ufundi hawakufurahishwa na matokeo ya kupoteza mechi dhidi ya Azam Fc hivyo wamepania kusahihisha makosa katika mchezo dhidi ya Prisons
Baada ya kumalizana na Prisons, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Simba, utapigwa May 08 katika uwanja wa Benjamin Mkapa