Beki kisiki wa Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' leo ataungana na wenzake jijini Mbeya wakijiandaa na mchezo wa hatua ya 16 bora kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Tanzania Prisons
Ninja hakusafiri na timu jana akiwa amepewa ruhusa kurejea visiwani Zanzibar kumaliza msiba wa dada yake
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema Ninja alicheza mechi dhidi ya Azam akiwa amefiwa hivyo walimruhusu kwenda kushiriki mazishi baada ya kumaliza mchezo huo
"Ninja alicheza mchezo wetu wa ligi dhidi ya Azam FC akiwa amefiwa hivyo aliomba amalize majukumu yake na kusafiri kwenda Zanzibar kwa ajili ya msiba hivyo tayari ameshamaliza na atajiunga na timu," alisema Bumbuli
Ninja amekuwa katika kiwango bora sana, sasa akiangaliwa kama mchezaji tegemeo katika safu ya ulinzi ya Yanga