Wiki iliyopita baada ya kumpokea Kocha Mpya wa Yanga Nasredinne Nabi, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Injinia Hersi Said alisema ujio wa Nabi ulikuwa ni mwanzo wa maboresho makubwa wanayokusudia kuyafanya pale msimu utakapomalizika
Hersi alisema maboresho yaliyofanyika msimu huu yalikuwa na manufaa pamoja na kuwa zipo changamoto zilizojitokeza ambazo wamekusudia kuziondoa katika usajili ujao
Katika mahojiano yake Injinia Hersi alikwenda mbali zaidi kwa kusema watavunja benki kwa maana ya kutumia fedha kusajili wachezaji watakaokuja kuimarisha zaidi timu
Mshauri wa Yanga Senzo Mazingisa anatajwa kuongoza kamati hiyo ya kuisuka Yanga imara zaidi
Ukiona moshi unafuka ni dalili ya moto! Jana msemaji wa Simba kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii aliwaomba mashabiki wamshawishi mmoja wa wachezaji wao akubali kusaini mkataba. Safari hii mwenye kisu kikali ndio atakula nyama!
Chini ya 'sterling' Senzo, kuna watu hawataamini macho yao kwani inakwenda kuundwa Yanga ile ambayo kila mmoja anaitamani
Habari njema zaidi ni kuwa hata mchakato wa Mabadiliko uko mbioni kukamilika ili kuruhusu muundo mpya wa uendeshaji
Mchakato ukikamilika maana yake utaruhusu Wawekezaji kuingiza fedha na hivyo kuwa na uwezo wa kufanya yote hayo yaliyokusudiwa