Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema kocha Juma Mwambusi bado yuko kwenye kikosi akiendelea na majukumu yake licha ya ujio wa kocha mkuu Nasredinne Nabi
Kumekuwa na sintofahamu juu ya hatma ya Mwambusi baada ya ujio wa Nabi ambaye amekuja na jopo lake la benchi la ufundi (Kocha Msaidizi, Kocha wa viungo)
Bumbuli amesema Mwambusi hakuwa ameonekana baada ya mchezo dhidi ya Gwambina Fc kwa sababu alikuwa akiuguliwa lakini alisimamia mazoezi ya jana sambamba na Nabi
"Mwambusi bado yupo Yanga isipokuwa juzi Jumanne alipata matatizo ya kifamilia ambapo aliomba ruhusa kwenda kuona mgonjwa. Lakini jana alikuwepo kambini, alisimamia mazoezi na kocha Nabi"
"Kocha wetu mpya bado hajapata vibali vya kufanya kazi nchini hivyo kimsingi bado majukumu yote ya timu yako chini ya Mwambusi"
"Bahati mbaya jana tukiwa kambini akapata taarifa kuwa mgonjwa amefariki hivyo anafanya utaratibu wa kwenda kuhudhuria msiba," alisema Bumbuli