Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said ametoa ufafanuzi wa makubaliano ya ushirikiano baina ya klabu ya Yanga na Raja Athletic baada ya kusainiwa mkataba hapo juzi
Injinia Hersi amebainisha maeneo ambayo Yanga itanufaika katika ushirikiano huo huku akisisitiza kuwa hakuna gharama yoyote ya fedha ambayo itatumika
Muungano huu utakwenda kugusa yafuatayo;
1. Ushirika wa kitaaluma
2. Ushirika wa ufundi na maendeleo ya vijana
3. Ushirika wa maandalizi na michezo ya kirafiki.
4. Ushirika wa taaluma za sheria, kidigitali, mauzo na masoko
Injinia Hersi amesema ushirikiano huo ni afya kwa maendeleo ya Yanga na Tanzania kwa ujumla
Raja Athletic ni miongoni mwa klabu kongwe barani Afrika ambapo mnamo mwaka 2013 iliweza kuwa klabu nambari 10 duniani kwa vigezo vya FIFA
Pia ilikuwa klabu nambari tatu Afrika kwa vigezo vya CAF katika KARNE ya 21