Wachezaji wa Yanga waliokuwa majeruhi wameanza kurejea kwenye kikosi wakiwa timilifu hivyo kufufua matumaini ya Yanga kutimiza malengo yake.
Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina ameweka bayana kuwa msimu huu Yanga inapigania kutwaa mataji yote inayoshiriki likiwemo kombe la mapinduzi linalotarajiwa kuanza wiki ijayo.
Baada ya Tshishimbi na Tambwe kurejea wakiwa fiti kwa asilimia 100, jana nahodha msaidizi Thabani Kamusoko alianza mazoezi mepesi yatakayoweza kumrejesha dimbani karibuni.
Donald Ngoma alipewa program maalumu ya mazoezi kwa muda wa wiki sita na anatarajiwa kurejea dimbani mwanzoni mwa mwezi Januari, 2018.
Kelvin Yondani yeye anasumbuliwa na kifundo wa mguu, majeraha aliyoyapata nchini Kenya kwenye michuano ya Chalenji, anatarajiwa kurejea dimbani wiki ijayo.
Kamati ya usajili wa Yanga ilisajili wachezaji wawili tu ikisisitiza ina imani na wachezaji waliopo (hasa washambuliaji) ambao wakati huo walikuwa majeruhi.
Kurejea kwa Tambwe, Kamusoko na Ngoma kutaifanya Yanga iimarike zaidi kutoka pale ilipofikia mzunguuko wa 11 ligi kuu ya Vodacom

ADVERTISE HERE