Wachezaji Tuisila Kisinda na Dickson Job leo walishindwa kumaliza mchezo dhidi ya Gwambina Fc baada ya kupata majeraha
Ukiwa ni mchezo wake wa pili tena akiwa katika kiwango bora, Job alipata majeraha na nafasi yake kuchukuliwa na Bakari Nondo Mwamnyeto
Kisinda alifanyiwa madhambi na mlinzi Gustapha Saimon na kuuangukia mkono wake, akapata majeraha yaliyomfanya ashindwe kuendelea na nafasi yake kuchukuliwa na Saido Ntibazonkiza

Ni bahati mbaya kwa nyota hawa kupata majeraha leo, Wananchi tunawaombea waweze kupona ili wawahi dabi ya Kariakoo May 08
ADVERTISE HERE