Mshambuliaji Ditram Nchimbi leo amekata ngebe za wakosoaji wake baada ya kufunga bao kali nje ya 18 katika ushindi wa mabao 3-1 ambao Yanga imepata dhidi ya Gwambina Fc
Nchimbi hakuwa amefunga bao kwa zaidi ya miezi 12 lakini wiki iliyopita akaahidi kuwa wakati wake wa kuzifumania nyavu umewadia
Ulikuwa mchezo mzuri Gwambina Fc wakitoa upinzani mkali kwa Yanga licha ya kuruhusu mabao matatu
Mabao mengine ya Yanga yalifungwa na Bakari Nondo Mwamnyeto na Saido Ntibazonkiza aliyefunga bao la tatu katika dakika za majeruhi


Hata hivyo Ntibazonkiza aliibua sintofahamu baada ya kuomba atoke muda mfupi baada ya kufunga bao hilo
Ntibazonkiza hakuanzishwa katika mchezo huo pengine jambo hilo halikumfurahisha licha ya kuwa bao lake la dakika za majeruhi liliihakikishia Yanga ushindi huo mnono
Ni matokeo ambao yameifanya Yanga iendelee kujichimbia juu ya msimamo wa ligi baada ya kufikisha alama 57
Mchezo utakaofuata ni dhidi ya Azam Fc na utapigwa Jumapili April 25 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kocha mpya wa Yanga Nasreddine Mohamed Nabi alishuhudia mchezo huo akiwa jukwaani na Mkurugenzi wa GSM Mhandisi Hersi Said